Tuesday, November 8, 2011

RAIS BARCELONA ATAKA IDADI NDOGO TIMU ZA LIGI KUU.

RAIS wa timu ya Barcelona ya Hispania Sandro Rosell amedai kuwa anahitaji Ligi Kuu ya nchi hiyo maarufu kama 'La Liga' kupunguza timu kutoka timu 20 ambazo ndio idadi ya sasa mpaka timu 16 na kuwawekea mipaka wawekezaji wa kigeni walionunua vilabu vya nchi hiyo. Barcelona na Real Madrid ndio wanaotawala ligi hiyo kwasasa na Rosell amesema klabu hizo mbili lazima zisaidie klabu zingine kupitia haki za matangazo ya televisheni na kwa kufanya hivyo itasaidia ligi za chini ziwe za ushindani zaidi. Barcelona na Madrid wametia saini mikataba yao wenyewe ya haki za matangazo ya televisheni hivyo kuzifanya kuchukua fedha nyingi zaidi kuliko timu zingine zinazoshiriki ligi hiyo. Rosell amesema wanatakiwa wakubaliane ndani ya miaka mitano kufuata mfumo wa Ligi Kuu ya Uingereza na kufanya mikataba ya haki ya matangazo ya televisheni kuwa sawa ili kila klabu ipate fungu la pamoja.

No comments:

Post a Comment