Monday, November 14, 2011

MISRI YAKUBALI KIPIGO CHA MABAO 2-0 DHIDI YA BRAZIL, HASSAN AWEKA REKODI.

KIUNGO mkongwe wa timu ya Taifa ya Misri Ahmed Hassan ameweka rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi za kimataifa baada ya kucheza mchezo wake wa 178 wakati timu yake ilikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Brazil katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika Doha, Qatar. Hassan ambaye ana umri wa miaka 36 alianza kukichezea kikosi hicho mapema mwaka 1995 akiwa na umri wa miaka 20 ambapo sasa amelingana na golikipa wa Saudi Arabia Mohamed Al Deayea ambaye alistaafu kucheza soka la kimataifa mwaka 2006. Kiungo huyo aliingia dakika ya 73 akichukua nafasi ya Hosni Abd Rabou na mara moja alikabidhiwa kitambaa cha unahodha alichokuwa amevaa Wael Gomaa.
Katika mchezo mshambuliaji anayechezea klabu ya Valencia ya Hispania Jonas ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya Brazil bao la kwanza akiwa amefunga dakika ya 39 kabla kumalizia linguine dakika ya 59.

No comments:

Post a Comment