Monday, November 14, 2011

UEFA KUWAJADILI MASHABIKI WAKOROFI WA CELTIC.

KAMATI Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA linatarajiwa kusikiliza kesi ya ushangiliaji mbaya uliokuwa ukifanywa na mashabiki wa klabu ya Celtic wakati wa mchezo Ligi ya Ulaya baina ya timu hiyo na Rennes. Kamati hiyo ya UEFA inatarajia kusikiliza kesi hiyo Desemba 8 mwaka huu ambapo katika mchezo baina ya timu hizo mashabiki w Celtic walisikika wakiimba nyimbo za kuchukiza katika mchezo huo ulifanyika Novemba 3 katika Uwanja wa Celtic Park. Uefa imesema katika shauri hilo hakutakuwa na umuhimu wa kuwepo kwa mwakilishi kutoka Celtic. Msemaji wa UEFA amesema kama ni kweli tuhuma hizo ni za kweli dhidi ya mashabiki hatua kali zitachukuliwa kwakuwa mambo hayo hayakubaliki mchezoni na inaweza kuvuruga amani.

No comments:

Post a Comment