Akizungumzia kuhusu timu yake kupoteza mchezo wa kwanza wakiwa nyumbani Saleh amesema walipoteza mchezo huo kwasababu walikuwa hawaifahamu Stars vizuri na mchezo huo umewasaidia kuwasoma vizuri na ana matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo wa kesho. Kama Stars wakifanikiwa kuibuka na ushindi ama sare ya aina yoyote katika mchezo huo wataingia hatua ya makundi ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Brazil 2014 wakiungana na za Morocco, Ivory Coast pamoja na Gambia katika kundi C.
Monday, November 14, 2011
STARS KATIKA KIBARUA KIZITO NA CHAD KESHO.
TIMU ya Soka ya Tanzania-Taifa Stars inatarajiwa kujitupa uwanjani kesho kupambana na timu ya Taifa ya Chad mchezo ambao utapigwa katika Uwanja Taifa, Dar es Salaam. Akizungumza Dar es Salaam leo, Kocha wa Stars Jan Poulsen alitamba kuwa kikosi cha kitaibuka na ushindi katika mchezo huo ingawa amekiri kuwa haitakuwa kazi rahisi pamoja na ushindi walioupata ugenini wa bao 2-1 wiki iliyopita. Amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri nzuri kwa ajili ya mchezo huo wa kesho na kuwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu hiyo. Nae Kocha wa Chad Habibu Mohamed Saleh amesema kuwa kikosi chake kimekuja kwa kazi moja tu kusaka ushindi ili waweze` kusonga mbele katika hatua ya makundi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment