Friday, November 11, 2011
PELE ASTUSHWA NA MAANDALIZI YALIYODORORA NCHINI BRAZIL.
MCHEZAJI nguli wa zamani Pele ameonyesha wasiwasi katika maandilizi ya michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kufanyika nchini Brazil 2014. Pele alilitetea Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA wa kuitaka Brazil kupitisha haraka sheria zinazohitajika kwa ajili michuano hiyo akidai walikuwa wanajua matakwa waliokuwa wakihitaji FIFA wakati wakitafuta nafasi ya kuandaa michuano hiyo. Pele ambaye ni balozi wa Kombe la Dunia nchini Brazil amesema anashangazwa na kuchelewa kwa miji 12 ambayo itaandaa michuano hiyo ikiwemo suala la ujenzi wa viwanja lakini akaongeza kuwa anaamini Brazil itafanya lolote liwezekanalo kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo ndani wakati. Pele alitoa kauli hiyo katika mkutano wa waandishi wa habari wakati akizindua taasisi ya uchunguzi wa watoto ambayo itatumia jina lake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment