Friday, November 11, 2011

VILLAS-BOAS ASHTAKIWA NA FA.

Meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas ameshtakiwa na chama cha soka cha England FA kwa matamshi aliyotoa kuhusu mwamuzi Chris Foy katika mchezo dhidi ya QPR. Kocha huyo kutoka Ureno amekiri kuwa alikuwa "mkali sana" kwa Foy, ambaye alimuonesha kadi nyekundu Jose Bosingwa na Didier Drogba na pia kuonesha wachezaji wengine saba wa Chelsea kadi za manjano. "Ana hadi Novemba 15 saa kumi alasiri kujibu mashtaka hayo." Bosingwa alitolewa kwa kumuangusha Shaun Wright Phillips na Drogba alipewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Adel Taarabt."Villas-Boas ameshtakiwa kwa uwajibikaji mbaya," imethibitisha taarifa ya FA. 
Chelsea walitozwa faini ya pauni 20,000 baada ya kukiri shtaka la kushindwa kuwadhibiti wachezaji wake. Akizungumza baada ya mchezo huo ambao Chelsea walifungwa 1-0, Villas-Boas, 34, ambaye yupo katika msimu wake wa kwanza kama meneja wa Chelsea alisema: "Mwamuzi alikuwa na kiwango kibovu sana. Imeonesha hadi kwenye matokeo ya mchezo. "Nilizungumza naye baada ya mchezo, na nilikuwa mkali sana. Sijali kama yuko sawa au la. "Yeyote anaweza kuwa na siku mbaya, lakini hii haikuwa siku mbaya kwetu, ilikuwa siku nzuri sana, na mbaya kwa mwamuzi." Alisema Villas-Boas.

No comments:

Post a Comment