Wednesday, November 2, 2011

REDKNAPP KUFANYIWA UPASUAJI MDOGO WA MOYO.


Klabu Tottenham Hotspurs imedhibisha kwamba kocha wake Harry Redknapp anatakiwa kufanyiwa upasuaji mdogo wa moyo. Redknapp-64- alikimbizwa hiospitali Jumanne usiku kwa ajili ya uchunguzi na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji huo mdogo katika moja ya mirija ambayo imeziba katika moyo wake. Kocha huyo ameshindwa kusafiri na kikosi cha timu yake kilichokwenda Urusi kwa ajili ya mchezo Ligi ya Europa dhidi ya Rubin Kazan utakaochezwa alhamisi ambapo timu hiyo ndio inayoongoza kundi A kwa pointi mbili mbele ya PAOK ya Ugiriki.
Kocha Msaidizi Kevin Bond na kocha wa kikosi cha kwanza Joe Jordan ndio watakuwa na majukumu ya kukiongoza kikosi hicho wakati Redknapp akipata matibabu.Kocha huyo aliliambia gazeti moja nchini Uingereza anaamini tatizo lake hilo halitamzuia kurudi kuitumikia timu hiyo Jumapili wakati wa mchezo wa ligi baina ya timu hiyo na Fulham.

No comments:

Post a Comment