Thursday, November 17, 2011

RIO ASHANGAZWA NA KAULI YA BLATTER KUHUSU UBAGUZI.

BEKI wa timu ya Taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United Rio Ferdinand amesema amshangazwa na madai ya Rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter akidai kuwa hakuna ubaguzi katika mchezo wa mpira uwanjani. Blatter alijichanganya katika kauli yake akzungumzia suala la ubaguzi uwanjani kuwa linaweza kutatuliwa kwa wachezaji kupeana mikono baada ya mchezo ingawa baadae alidai kuwa ameeleweka vibaya. Katika mtandao wa kijamii wa Twitter Ferdinand aliandika ujumbe wa kuonyesha kushangazwa na kauli hiyo kwa kusema kuwa anaweza kuwa amekosea kusoma matamshi ya Blatter aliyotoa na kama hajakosea kosea kusoma basi ameshangazwa na kauli ya kiongozi huyo. Ferdinand baadae alimtumia ujumbe kwa Blatter. Katika ujumbe huo aliosema kuwa matamshi yake kuhusiana na ubaguzi yanashangaza na kwa kweli yanachekesha na iwapo mashabiki watapaza sauti zao kwa maneno ya kibaguzi jee kushikana mikono hapo ni sawa? Matamshi ya Blatter yamekuja wakati nahodha wa Chelsea John Terry akichunguzwa na polisi pamoja na Chama cha Soka cha Uingereza-FA juu ya tuhuma za kumtamkia maneno ya kibaguzi mlinzi wa QPR Anton Ferdinand, ambaye ni mdogo wake Rio.

No comments:

Post a Comment