Thursday, November 17, 2011

28 WAITWA KILIMANJARO STARS.

KOCHA Msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Bara-Kilimanjaro Stars Jamhuri Kihwelu ametaja majina ya wachezaji 28 watakaounda kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Challenge yanayotarajiwa kuanza Novemba 25 mpaka Desemba 10 mwaka huu. Akizungumza Dar es Salaam, kocha huyo amesema kikosi hicho kinatarajiwa kuweka kambi Ijumaa Novemba 18 katika Hoteli ya Rainbow ambapo watakaa hapo kwa muda wa wiki moja kabla kufanya mchujo na kubakiwa na wachezaji 20 wataounda kikosi hicho. Amesema katika kikosi hicho kutakuwa na makipa Juma Kaseja ambaye atakuwa nahodha wa kikosi hicho, Deo Mushin na Shaban Kado mabeki ni Shomari Kapombe, Godfrey Taita, Juma Jabu, Paulo Ngelema, Erasto Nyoni, Salum Telela na Juma Nyoso. Viungo watakuwa ni Shaaban Nditi, Ibrahim Mwaipopo, Nurdin Bakari, Mwinyi Kazimoto, Haruna Moshi, Ramadhani Chombo, Jimmy Chogy, Mohamed Sudi, Nizar Khalfan, Rashid Yusuph na Said Morad wakati washambuliaji watakuwa ni Mrisho Ngassa, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, John Bocco na Gaudence Mwaikimba, Hussein Javu na Daniel Ruben.

No comments:

Post a Comment