Friday, November 18, 2011

CLUB WORLD CUP: BARCA KUKUTANA NA MABINGWA WA AFRIKA.

MABINGWA wa soka barani Ulaya klabu ya Barcelona inatarajia kupambana na mshindi kati timu ya Esperance au Al-Sadd katika nusu fainali ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia. Ratiba hiyo ilipangwa Alhamisi ambapo kikosi cha Barcelona kinachoongozwa na kocha Pep Guardiola kitapambana na aidha Esperance kutoka Tunisia ambao ni mabingwa wa Afrika au Al- Sadd ya Qatar ambao ni mabingwa wa bara la Asia. Rais wa Esperance Riadh Bennour amesema ratiba hiyo ni nzuri pamoja na kwamba watu wengi wanategemea kuona mchezo wa fainali ya michuano hiyo zicheze timu za Barcelona na Santos ya Brazil. Aliongeza pamoja na watu kutegemea hivyo wao watajaribu kufanya kila wawezalo kuhakikisha wanaingia fainali na kucheza na timu mojawapo kati ya hizo. Michuano hiyo ambayo hukusanya viabu bingwa kutoka katika kila bara duniani inatarajiwa kufanyika Japan katikati ya mwezi Desemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment