Wednesday, November 16, 2011

ROAD TO BRAZIL: TANZANIA, KENYA, UGANDA ZAFUZU HATUA YA MAKUNDI.

Golikipa wa timu ya Chad akijaribu kuokoa mpira uliopigwa na mshambualiaji wa Taifa Stars Thomas Ulimwengu katika baina ya timu hizo ulichezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
TIMU za Taifa za Tanzania, Kenya na Rwanda zimefuzu kuingia katika hatua ya makundi katika kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Licha ya Taifa Stars kufungwa bao 1-0 na Chad katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam timu hiyo imesonga mbele kwa akiba nzuri ya bao la ugenini iliyopata katika mchezo wao wa kwanza. Kenya Harambee Stars imesonga mbele kwa idadi ya mbao 7-0 katika michezo miwili waliyocheza na Shelisheli baada ya mchezo wa kwanza kuishindilia timu mabao 4-0 kwao kabla ya kumalizia kwa mabao 3-0 jana katika Uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi. 
Mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo wa Taifa Stars na Chad.
Michezo mingine iliyochezwa jana ni Rwanda iliibamiza Eritrea kwa mabao 3-1 na kusonga mbele kwa idadi ya mabao 4-1 katika michezo miwili waliyocheza, Equatorial Guinea nayo ilisonga mbele licha kipigo cha mabao 2-1 walichokipata jijini Antananarivo. wakati Jamhuri ya Didemokrasia ya Kongo-DRC wao waliendeleza ubabe kwa timu ya Swaziland kwa kuichapa mabao 5-1 jijini Kinshasha na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 8-1.

No comments:

Post a Comment