Wednesday, November 16, 2011

EURO 2012: URENO, CZECH REPUBLIC NA CROATIA ZAFUZU.

TIMU za taifa za Ureno, Czech Republic na Croatia zimefuzu kucheza michuano ya Ulaya inayotarajiwa kufanyika mwakani. Ureno walifuzu kucheza michuano hiyo kwa kuifunga Bosnia mabao 6-2 katika michezo miwili waliyocheza wakati Jamhuri ya Czech wao walifuzu baada ya kuifunga Montenegro mabao 3-0 katika michezo miwili waliyocheza. Pamoja na Suluhu ya bila ya kufungana waliyopata Croatia dhidi ya Uturuki nchi hiyo ilisonga mbele baada ya kupata ushindi mnono 3-0 katika mchezo wa kwanza jijini Istanbul wakati Jamhuri ya Ireland nao waliingia katika michuano hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Estonia na kutimiza idadi ya mabao 5-1 katika michezo miwili waliyokutana. Mbali ya hizo nchi nyingine ambazo zimeshafuzu kucheza michuano hiyo ni pamoja na Poland na Ukraine ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo nyingine ni Ujerumani, Urusi, Italy, Ufaransa, Uholanzi, Uingereza, Denmark, Hispania na Sweden.

No comments:

Post a Comment