TOURE KUKATWA MSHAHARA WA WIKI SITA.
|
Kolo Toure |
BEKI wa Manchester City Kolo Toure amekatwa mshahara wa wiki sita na klabu yake hiyo kufuatia kukutwa na hatia ya kutumia dawa zilizokatazwa michezoni. Toure alifungiwa kutocheza mpira kwa muda wa miezi sita mwezi Mei adhabu ambayo alipewa na Shirika la Kimataifa ya kupinga dawa hizo michezoni baada kugundulika kutumia dawa hizo ambazo zilikuwa za mkewe ili zimsaidie kupunguza uzito. Klabu hiyo nayo iliamua kumchukulia hatua mchezaji huyo lakini walisubiri kwanza amalize adhabu aliyopewa na shirikka hilo la dunia imalizike. Sasa klabu hiyo imeamua kumkata mchezaji huyo mshahara wake wa wiki tatu ambao unafikia kiasi cha paundi 720,000, lakini cha muhimu ni kwamba wameamua kutochukua haki zake za matangazo ambazo zina thamani ya paundi milioni 1.5. Taarifa ya klabu hiyo imesema mchezaji huyo amekubali adhabu hiyo na sasa wanaweza kufunga mjadala huo na kuendelea na mbele.
No comments:
Post a Comment