Tuesday, November 8, 2011

FIFA YAICHOMOLEA UINGEREZA KUVAA RIBONI ZA KUWAKUMBUKA MASHUJAA WAO WA VITA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limekataa tena ombi la Chama cha Soka nchini Uingereza-FA kuvaa ua jekundi katika jezi za timu hiyo wakati wa mchezo wao Jumamosi dhidi ya Hispania. FA waliomba ruhusa kutoka FIFA kuvaa viua hivyo ili kukumbuka mashuja wao waliokuwa vitani. Lakini FIFA imesema katika ripoti yake kuiruhusu nchi hiyo kufanya hivyo kutafungua milango kwa nchi nyingine nazo kuomba kufanya hivyo hali ambayo itapelekea kupoteza uhalisia na mvuto wa mchezo huo. Wakiwa kama wasimamizi wa masuala ya mpira duniani waliweka sheria ya kuwa jezi wanazovaa wachezaji hazitakiwi kuwa na nembo inayohusiana na masuala ya siasa, dini au biashara. FIFA wameruhusu dakika moja ya ukimya kwa ajili ya kuwakumbuka mashujaa hao katika mchezo baina ya Uingereza na Hispania ambao utachezwa katika Uwanja wa Wembley ambayo itakuwa ni siku moja kabla ya siku ya kuwakumbuka mashujaa hao Jumapili.

No comments:

Post a Comment