Tuesday, November 8, 2011

"REKODI SIO MUHIMU KWANGU KULIKO VIKOMBE." MESSI.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona Lionel Messi amefafanua kuwa sio matarajio yake kuwa mfungaji anayeongoza mabao aliyepata kutokea katika klabu hiyo bali anachotaka yeye ni kufanya vizuri kadri ya uwezo wake kuisaidia klabu hiyo. Akihojiwa na gazeti moja nchini Hispania Messi amesema anahitaji kuvunja rekodi ya Rodrigez lakini tu ni kwasababu anahitaji kufunga mabao mengi kwa ajili ya klabu hiyo ili aweze kuisadia kushinda vikombe zaidi na hajali kuhusu suala la kuingia katika rekodi ya klabu. 
Mapema msimu huu mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alichupa mpaka nafasi ya pili kwa ufungaji katika historia ya klabu hiyo akichukua nafasi ya Ladislao Kubala na amebaki Cesar Rodrigez pekee akiwa ameshinda mabao 235 ndio anayemzidi Messi. Hatahivyo Messi mwenye umri wa miaka 24 amesisitiza kuwa kuvunja rekodi sio muhimu kama kushinda vikombe lakini kama ikitokea hivyo ni sawa tu ingawa kitakuwa sio kitu kitachomkosesha usingizi. Messi mpaka sasa ameshafunga mabao 203 toka ajiunge na klabu hiyo mwaka 2005.

No comments:

Post a Comment