Tuesday, November 8, 2011

ADEBAYOR KUREJEA TIMU YA TAIFA.

BAADA ya miezi kadhaa ya Shirikisho la Soka la Togo-FTF kumuomba nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya nchi hiyo Emmanuel Adebayor kurejea katika kikosi baada ya kujitoa kufuatia tukio la kuvamiwa lililopata timu hiyo mjini Cabinda ameamua kurejea rasmi katika kikosi hicho. Adebayor amerejea katika kikosi hicho ili kukisaidia kujianda na kutafuta tiketi ya michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika mwaka 2013 pamoja ile ya Kombe la Dunia itayochezwa mwaka 2014. Chanzo kimoja kutoka ndani ya FTF kilisema Mwenyekiti wa shirikisho hilo Gabriel Ameyi ambaye wiki aliyopita alitangaza kwenda jijini Landon kuzungumza na mchezaji huyo anayecheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs alihahirisha na badala yake alizungumza naye kwa simu mazungumzo ambayo amedai yamekwenda vizuri. Shirikisho hilo litatangaza rasmi hivi karibuni kurejea kwa mchezaji huyo baadaye kidogo, Adebayor angependa kuitwa katika kikosi hicho kwa ajili ya mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia utakaochezwa nyumbani na ugenini Novemba 11 na 15 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment