KIUNGO wa kimataifa wa Kenya Jerry Santos amesema Ligi Kuu ya nchini Kenya ina ushindani zaidi kutofautisha na Ligi Kuu Tanzania bara. Santos amesema hayo katika mahojiano maalumu na mtandao wa Supersport baada ya kuthibisha kuachana na klabu ya Simba mara baada ya mkataba wake kumalizika wiki iliyopita. Mchezaji huyo anayecheza nafasi ya kiungo amesema alikuwa na mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo na kwasasa hana klabu yoyote lakini amemwachia suala hilo meneja wake kumtafutia klabu nyingine. Santos aliendeleakusema kuwa bado Simba walionyesha nia kumhitaji kwa kutaka kumuongeza mkataba mwingine lakini akasema mpaka hapo watapoamua kutuma maombi yao kwa maandishi anaweza kukubali ofa hiyo.
Amesema alifurahi katika kipindi chote alichokuwa akicheza Tanzania na kwamba tofauti kati ya ligi hizo mbili ni kwamba klabu za Tanzania zinalipa vizuri zaidi ya kwao na Tanzania ni kwamba huku wanalipa vizuri tofauti na ligi ya kwao ingawa alikiri kuwa ligi yao ina ushindani zaidi tofauti na Tanzania.
No comments:
Post a Comment