VIWANJA mbalimbali barani Afrika vinatarajiwa kutimua vumbi Ijumaa Novemba 11 ambapo timu kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika zitapambana ili kupata nafasi ya kuingia katika hatua ya makundi ya timu zinatakzotafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia 2014 itakayofanyika Brazil.
Katika michezo hiyo timu ya Taifa ya Tanzania-Taifa Stars ambayo imeondoka nchini jana jioni itakuwa wageni wa timu ya Taifa ya Chad katika mchezo utaopigwa katika jiji la N'Djamena mchezo utakaochezwa saa tisa za jioni kwa sasa za huko ambapo kwa hapa Tanzania itakuwa saa kumi na mbili jioni.
Michezo mingine itakayochezwa siku hiyo ni pamoja na Shelisheli itaikaribisha Kenya, Guinea Bissau itakuwa mwenyeji wa Togo jijini Bissau, Djibouti itaikaribisha Namibia, Visiwa vya Comoro wataikaribisha Msumbiji, Equatorial Guinea itachuana na Madagascar na Lesotho itaikaribisha Burundi. Michezo mingine ni Eritrea wataikaribisha Rwanda jijini Asamara, Swaziland watachuana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sao Tome e Principe itapambana na Congo Brazzaville wakati Jumamosi kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Somalia na Ethipiopia.
No comments:
Post a Comment