Wednesday, November 9, 2011

TUSKER CHALLENGE CUP: TANZANIA BARA YAPANGWA NA RWANDA, ETHIOPIA NA DJIBOUTI, ZANZIBAR KUIKWAA UGANDA, BURUNDI NA SOMALIA.

Baraza michezo la nchi za Afrika Mashariki na Kati-CECAFA limetangaza makundi ya timu zitazoshiriki michuano ya Kombe la Challenge inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Novemba 15 mwaka huu. Akizungumza wakati wa kupanga makundi ya timu zitakazoshiriki michuano hiyo Mwenyekiti wa CECAFA Leodgar Tenga amesema michuano hiyo itashirikisha timu 12 ambazo zitagawanywa katika makundi matatu. Amesema kundi A kutakuwa na timu za Tanzania ambao ni wenyeji wa michuano hiyo, Rwanda, Ethiopia na Djibout, kundi B litakuwa na timu za Uganda, Burundi, Zanzibar na Somalia wakati kundi C ambalo linahesabika kama kundi la kifo litakuwa na timu za Sudan, Kenya, Malawi ambaye ni timu mwalikwa katika michuano hiyo na Eritrea. Tenga amesema ili kufanikisha michuano hiyo kiasi cha shilingi bilioni 1.4 kinahitajika ambapo mpaka sasa ni kiasi cha shilingi milioni 823 ndio kilichopatikana hivyo kuomba wadhamini wengine kujitokeza kwa wingi kusaidia kifanikisha michuano hiyo. Ratiba kamili ya michuano hiyo inatarajiwa kutoka Jumamosi hii ambao Viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam na CCM Kirumba jijini Mwanza ndio vinavyotarajiwa kuchezewa michuano hiyo. Tenga amesema timu mbalimbali ziliomba kushiriki michuano hiyo kama Ivory Coast , Zambia, Botswana na Ghana lakini kutokana kushiriki kwao michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakayofanyika Januari mwakani, wakashindwa kuteua moja ya timu hizo kutoka muda kuwa mchache.

No comments:

Post a Comment