|
David Cameron, Waziri Mkuu wa Uingereza akiwa amevalia kiua hicho kinacholeta utata. |
SAKATI la timu ya Taifa ya Uingereza kukataliwa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA kuvaa ua jekundu katika jezi zao katika mchezo wa kirafiki siku ya Jumamosi limechukua sura mpya baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo David Cameron kuingilia kati suala hilo. Cameron ameitaka FIFA kuangalia upya suala hilo baada ya shirikisho hilo kukikatalia Chama cha Soka cha nchi hiyo mara mbili ombi lao hilo. Waziri Mkuu huyo amesema wazo la kuvaa viua hivyo katika jezi zao ili kuwakumbuka mashujaa wao walipigania uhuru kuwa ni suala la kisiasa ni ngumu kuelewa. Cameroon akaendelea kusema kuwa kuwa kuvaa viua hivyo ni heshima kubwa na kitu cha kijuvunia kwa taifa hilo. FIFA iliweka wazi kuwa jezi ya mchezaji hairuhusiwi kubeba ujumbe wowote unaohusiana na masuala ya kisiasa, dini au kibiashara. Shirikisho hilo lilifanua kuwa kuiruhusu Uingereza kufanya hivyo kutafungua milango kwa mataifa mengine duniani kufanya kitu kama hicho hivyo kuondoa ladha na uhalisia wa mchezo wa soka. Hata hivyo FIFA wameruhusu timu hizo kukaa kimya kwa dakika moja wakati wa mchezo huo ambao utachezwa Jumamosi ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya kukumbuka mashujaa hao Jumapili.
No comments:
Post a Comment