Thursday, November 10, 2011
FIFA YAFYATA MKIA KWA UINGEREZA.
HATIMAYE Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limekubali nchi za Uingereza, Scotland na Wales timu zao za Taifa kufunga vitambaa vyeusi mkononi badala ya ua jekundu wakati wa michezo yao ya kimataifa ya kirafiki mwishoni mwa wiki hii. Kauli hiyo imekuja baada ya Prince William na Waziri Mkuu wan chi hiyo David Cameron kulivalia njuga suala hilo kwa kuitaka FIFA kuiruhusu nchi hiyo kuvaa ua jekundu katika jezi zao. Shirikisho hilo lilikataza nchi yoyote kuvaa nembo inayohuasiana na masuala kisiasa, dini au biashara katika jezi zao. Uingereza na Wales wamekubaliana na suala hilo wakati Scotland wanasubiri mpaka hapo watapozungumza timu watayocheza nayo ya Cyprus kabla ya kutoa uamuzi wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment