Thursday, November 10, 2011

NEYMAR KUSAINI MKATABA MPYA NA SANTOS.

RAIS wa klabu ya Santos ya Brazil Luiz Alvaro Ribeiro amesema kuwa mshambuliaji wa timu hiyo Santos amekubali kusaini mkataba mpya ambao utamuweka katika klabu hiyo mpaka 2014 wakati nchi hiyo itapokuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia. Ribeiro amesema waliafikia na mchezaji huyo kuhusu mkataba wake mpya JUmatano lakini alikataa kusema ni kiasi gani watakuwa wakimpa. Hivi karibuni mchezaji huyo amesema kwamba anahitaji kubakia nchini Brazil kwa mmoja zaidi baada ya tetesi kuwa vilabu vikubwa barani Ulaya kama Real Madrid na Barcelona kwamba zilikuwa zikifanya nae mazungumzo.

No comments:

Post a Comment