Monday, November 21, 2011

VILLAS-BOAS ADAI ANA UHAKIKA NA KIBARUA CHAKE.

MENEJA wa Chelsea Andre Villas-Boas amesisitiza kuwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich bado ana imani nae katika mipango ya muda mrefu pamoja na kupoteza michezo mitatu ya ligi kati ya minne waliyocheza. Mapema Jumapili uongozi wa Chelsea ulilaani vikali baadhi magazeti kuandika kuwa kuna nyufa zimejitokeza baina ya kocha huyo na uongozi wa klabu hiyo. Ambapo baada ya kipigo walichokipata kutoka kwa Liverpool cha mabao 2-1 kocha huyo amesema ana uhakika wa kibarua chake kwakuwa Abromovich hakulipa kiasi cha paundi milioni 13 kumuondoa katika klabu yake ya zamani ya Porto halafu alipe tena mihela hiyo kumuondoa katika klabu hiyo. Aliendelea kusema kuwa hilo sio suala la mmiliki huyo kuwa na subira kwakuwa walishazungumza kuwa wanatengeza kitu kipya katika klabu hii kwa ajili ya baadae. Baada ya kupoteza mchezo huo sasa Chelsea wako nyuma kwa alama 12 kwa vinara wa ligi hiyo Manchester City na Villas-Boas amekiri kuwa wana kazi kubwa ya kufanya ili kuweka matumaini hai ya kunyakuwa kombe hilo.

No comments:

Post a Comment