Monday, January 9, 2012

BARCELONA YATELEZA.

TIMU ya Barcelona jana imeteleza na kuachwa kwa tofauti ya pointi tano nyuma ya mahasimu wao wanaongoza Ligi Kuu nchini Hispania Real Madrid baada ya kukubali sare ya bao 1-1 dhidi ya Espanyol mchezo uliofanyika Jumapili. Mabingwa hao watetezi ambao msimu huu wamekuwa na wakisuasua katika michezo yao ya ugenini walikuwa wakijaribu kutafuta ushindi dhidi ya wapinzani wao hao wanaotoka katika jiji moja nchini humo ili waweze kupunguza tofauti ya pointi na vinara Madrid. Hali haikuwa hivyo kwani Espanyol nao walijizatiti vilivyo kuhakikisha wanaondoka na pointi na kuifanya Barcelona kuwa na pointi 38 katika michezo 17 waliyocheza huku vinara wa ligi hiyo Madrid wakiwa na pointi 43 katika michezo 17 waliyocheza baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Granada kwa mabo 5-1 Jumamosi. Akihojiwa na vyombo vya habari mara baada ya mchezo huo meneja wa Barcelona Pep Guardiola amesema kuteleza katika mchezo huo sio kwamba ligi ndio imekwisha na la muhimu kwao ni kuangalia wapi wamekosea ili wafanye vizuri katika michezo mingine.

No comments:

Post a Comment