Monday, January 9, 2012

RODRIGUEZ AKIRI KUUNAWA MPIRA.

Mchezaji wa Espanyol Raul Rodriguez amekiri kuwa alizuia mpira kwa mkono wakati timu yake ilipotoa sare ya bao 1-1 na Barcelona mchezo uliofanyia Jumapili. Wakati mchezo ukielekea dakika za mwisho Rodriguez alizuia shuti alilopiga mchezaji wa Barcelona Pedro kwa mkono kitendo ambacho kingeweza kumsababishia mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya njano na penati kwa Barcelona. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Rodriguez alikiri kuwa ni kweli mpira ulimpiga mkononi lakini akadai kuwa yeye hakuwa mwamuzi. Aliendelea kusema kuwa sare hiyo walioipata imewaongezea kujiamini zaidi na ana imani wataendelea kufanya vizuri zaidi katika michezo yao inayofuata.

No comments:

Post a Comment