Monday, January 9, 2012

BENFICA YAKAMATA USUKANI URENO.

TIMU ya Benfica imekamata usukani wa Ligi Kuu nchini Ureno baada ya kuibuka na uhindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Leiria na kujichimbia kileleni wakiwa na tofauti ya pointi mbili nyuma ya mabingwa watetezi FC Porto. Benfica ambao haijafungwa toka msimu huu wa ligi hiyo uanze walikuwa wamefungana pointi na Porto toka mwezi Octoba mwaka jana lakini walipata nafasi ya kuiacha timu hiyo baada ya kutoa suluhu ya bila ya kufungana na Sporting. Mabao ya Benfica yaliwekwa kimiani na Bruno Cesar katika dakika ya 10 huku mshambuliaji wake Oscar Cardozo akiomngeza la pili dakika ya 48 kabla ya Rodrogo Moreno kufunda mawili katika dakika za majeruhi. Pia katika michezo mingine iliyochezwa Jumapili ni pamoja na Maritimo ilifanikiwa kuifunga Olhanense mabao 2-1, Rio Ave iliifunga Pacos de Ferreira bao 1-0, Gil Vecente ilikubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Nacional na Guimaraes ilishinda bao 1-0 dhidi ya Feirense.

No comments:

Post a Comment