Wednesday, January 4, 2012
EUSEBIO ARUDISHWA HOSPITALI.
MCHEZAJI nguli wa zamani wa Ureno Eusebio amerejeshwa tena hospitali kwa matibabu baada ya siku chache za kuruhusiwa kwake baada ya matibabu ya ugonjwa wa pneumonia. Katika taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Da Luz iliyopo jijini Lisbon alipolazwa Eusebio imesema kuwa nyota huyo wa zamani alifikishwa hospitalini hapo Jumanne usiku akiwa anasumbuliwa na maumivu ya shingo. Eusebio aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo Jumamosi iliyopita na kupata matibabu yaliyochukua wiki mbili ikiwemo siku kadhaa alizokaa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuathirika mapafu yake yote mawili kutokana na pneumonia na doktari aliyemtibu alidai kuwa amepona. Mchezaji huyo ambaye jina lake kamili anaitwa Eusebio da Silva Ferreira atatimiza miaka 70 baadae mwezi huu na amekuwa nyota wa Ureno kutokana na uwezo wake mkubwa kusakata kabumbu aliouonyesha katika miaka 60 na Shirikisho la Soka la Duniani-FIFA kumtaja kama moja kati ya wachezaji 10 bora waliowahi kutokea duniani mwaka 1998.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment