Wednesday, January 4, 2012

GUINEA YAANZA MAANDALIZI YA AFCON 2012.

TIMU ya taifa ya Guinea imeanza maandalizi ya kujiwinda kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika iliyoandaliwa kwa pamoja na Gabon na Equatorial Guinea inayotarajiwa kuanza Januari 21 mwaka huu. Timu iliingia kambini mapema Jumatatu katika jiji la Conakry na kuanza mazoezi yake katika Uwanja wa September 28 ambayo yalihudhuriwa karibu na wachezaji wote wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi. Mojawapo ya wachezaji walihudhuria mazoezi ya timu hiyo inayonolewa na kocha Michel Dussuyer ni pamoja na Aziz Abdul Keita, Naby Yatara, Ibrahima Sory Conte, Boubacar Diallo, Djoulde Bah, Naby Soumah, Ousmane Barry, Ismael Bangoura, Ibrahima Sory Bangoura na Ibrahima Traore. Wachezaji ambao hawakujiunga na wenzao katika kambi hiyo ni Jean Habib Balde, Thierno Bah, Dian Bobo Balde na Pascal Feindouno lakini walitarajiwa kujiunga na timu hiyo mwishoni mwa wiki hii.

No comments:

Post a Comment