Monday, January 2, 2012

MOURINHO: SITASAJILI DIRISHA DOGO

MENEJA wa Real Madrid Jose Mourinho amesema kuwa hahitaji kumuacha mchezaji yoyote katika kipindi cha dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa baadaye mwezi huu. Akihojiwa na gazeto moja nchini Ureno Mourinho amesema katika kipindi hiki hahitaji kusajili mchezaji yoyote na tayari ameuambia uongozi wa klabu hiyo kuwa pia hahitaji kumuacha mcheza yoyote yoyote.
Mourinho aliendelea kusema kuwa wachezaji wanajua hilo na pia bodi ya wakurugenzi wa klabu pia wanajua hilo kuwa nahitaji kumaliza msimu huu nikiwa na kikosi hikihiki. Madrid ambao kwasasa ndio wanaoongoza msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania wanakabiliwa na mchezo mgumu ugenini dhidi ya Malaga mchezo ambao ni wa Kombe la Mfalme.

No comments:

Post a Comment