Monday, January 2, 2012

ROONEY ATOZWA FAINI.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Wayne Rooney ametozwa faini ya mshahara wake wa wiki moja na klabu yake hiyo baada ya kutoka kusheherekea sikukuu ya Chrismas na rafiki zake wiki iliyopita. Rooney aliachwa katika kikosi cha United ambacho kilipata kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Blackburn Jumamosi iliyopita kwa madai ya sababu za kiafya. Lakini magazeti ya nchini humo yaliripoti kuwa mshambuliaji huyo aliachwa kutokana na kushindwa kufanya mazoezi kwa kiwango kizuri Desemba 27 hali iliyotokana na kukesha akisherekea na mkewe Coleen pamoja na wachezaji wenzake Jonny Evans na Darron Gibson kitendo ambacho kilikuwa kinyume na matakwa ya klabu hiyo. Kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa na magazeti hayo imesema Rooney amepigwa faini in ayokadiriwa kufikia kiasi paundi 200,000 pamoja na beki wa timu hiyo Evans na kiungo Gibson.

No comments:

Post a Comment