Wednesday, January 4, 2012

SUAREZ AOMBA RADHI.

MSHAMBULIAJI wa Liverpool Luis Suarez ameomba msamaha baada ya kupewa adhabu ya kufungiwa mechi nane kwa kosa la kumtolea maneno ya kibaguzi beki wa Manchester United Patrice Evra. Katika taarifa ya klabu ya Liverpool imesema kuwa wamekubali adhabu ya mchezaji huyo kwa kumuita Evra neon ambalo lina ishara za kibaguzi lakini mchezaji huyo ameendelea kusisitiza kuwa hana kosa. Lakini taarifa ya mchezaji huyo aliyoitoa mapema leo amesema kuwa hakutumia neno hilo kwa nia ya kumuumiza yoyote na kama amemkwaza mtu kwa kutamka neno hilo anaomba msamaha na hata litumia neno hilo tena akiwa uwanjani nchini Uingereza. Mchezaji huyo alianza kuitumikia adhabu yake hiyo ya kufungiwa mechi nane Jumanne hii ambapo aliishuhudia timu yake ya Liverpool ikipokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka vinara wanaoongoza ligi hiyo Manchester City.

No comments:

Post a Comment