Monday, January 2, 2012

TUNISIA YATOA SULUHU NA BARCELONA.

TIMU ya taifa ya Tunisia imemaliza kambi yake ya maandalizi waliyoweka katika jiji la Barcelona nchini Hispania kwa kutoa suluhu ya bila ya kufungana na timu hiyo katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Olimpiki na kuhudhuriwa na mashabiki wapatao 35,000. Katika mchezo wake mwingine wa majaribio Tunisia walifanikiwa kuifunga Basques kwa mabao 2-0 mabao ambayo yaliwekwa kimiani na wachezaji Ihab Msakni na Adil Chedli. Kikosi cha Barcelona ambacho walitoa nacho suluhu kilikuwa kimejumuisha wachezaji kama Victor Valdes, Cesc Fabregas, Xavi Hernandez, Sergeo Busquets, Gerard Pique, Fontas, Montoya na Cuenca. Makocha wa timu zote mbili walijitahidi kutumia wachezaji wake wa kutegemewa lakini hakuna mabao yaliyopatikana ingawa kila mmoja alijitahidi kutengeneza nafasi za kufunga katika mchezo huo. Tunisia sasa itasafiri mpaka Falme za kiarabu kumalizia kambi yao kabla ya kuelekea Gabon katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayotarajiwa kuanza Januari 21 wakiwa katika kundi moja na wenyeji Gabon, Morocco na Niger.

No comments:

Post a Comment