Monday, February 13, 2012

ANZHI YAMTIMUA KOCHA WAKE.

KLABU ya Anzhi Makhachkala ua Urusi imemtimua kocha wake Yuri Krasnozhan baada ya kuinoa klabu hiyo kwa zaidi ya mwezi mmoja tu. Krasnozhan mwenye umri wa miaka 48 alijiunga na klabu hiyo mwishoni mwa mwaka uliopita baada ya kutimuliwa na klabu ya Lokomotiv Moscow mapema msimu huu pamoja na na kuyiwezesha klabu hiyo kuongoza katika kipindi hicho. Akihojiwa na mtandao wa klabu kocha huyo amesema kuwa sababu kubwa ya kuondoka kwake ni kushindwa kuelewana uongozi katika baadhi ya mambo ya klabu hiyo. Hatahivyo vyombo vya habari vya nchi hiyo vinasema kwamba sababu halisi ya kuondoka kwa kocha huyo ni kushindwa kuongoza wachezaji wenye majina makubwa katika timu hiyo kama mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto’o na beki wa kimataifa wa zamani wa Brazil Roberto Carlos. Pia kuna taarifa nyingine kuwa Fabio Capello ndio anatarajiwa kuchukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo ambapo Muitaliano huyo ambaye ameachia kibarua cha kuinoa Uingereza wiki iliyopita alikuwepo nchini humo mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya mazungumzo ya kuinoa klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment