Monday, February 13, 2012

CAF YATOA RAMBIRAMBI KWA WAATHIRIKA MISRI.

SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF limetoa kiasi cha dola 150,000 kwa familia za waathirika ya watu ambao walikumbwa katika vurugu zilizotokea uwanjani nchini Misri. Rambirambi hizo kutoka CAF zilipitishwa katika kikao ilichokaa Jumamosi katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon huku Shirikisho la Soka Duniani-FIFA nalo limesema litatoa kiasi cha dola 250,000 kwa ajili ya familia za waathirika. Bendera zimekuwa zikipepea nusu mlingoti latika michuano hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya Gabon na Guinea ya Ikweta na pia kumekuwepo na dakika moja za maombolezo katika kila mchezo. Vurugu hizo zilitokea baada ya mchezo wa Ligi Kuu nchini Misri ulifanyika jijini Port Said Februari 1 mwaka huu ambapo zaidi ya watu 70 walipoteza maisha katika vurugu hizo.

No comments:

Post a Comment