Wednesday, February 1, 2012

FULHAM YAMNYAKUWA MSHAMBULIAJI WA URUSI.

Pavel Pogrebnyak
Klabu ya Fulham imenyakuwa mshambuliaji wa kimataifa wa Urusi Pavel Pogrebnyak kutoka klabu ya Stuttgart na kumuuza mchezaji wake Bobby Zamora kwa mahasimu wao jijini London klabu ya Queens Park Rangers katika kipindi cha mwisho cha usajili wa dirisha dogo la usajili jana. Pogrebnyak mwenye umri wa miaka 28 amejiunga na Fulham kwa mkataba wa miezi sita ambapo alikuwa sehemu ya kikosi cha Urusi kilichoongoza kundi B katika kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya itakayofanyika baadae mwaka huu. Uhamisho huo umemuwezesha Zamora kujiunga na kocha wake wa zamani Mark Hughes katika klabu ya QPR. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amesaini mkataba wa miaka miwili na nusu na QPR ambapo sas atacheza pamoja na mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Djibril Cisse ambaye nae alikamilisha taratibu za uhamisho mapema jana.

No comments:

Post a Comment