AMOROS APEWA MKATABA WA MIAKA MIWILI.
|
Manuel Amoros |
BEKI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa Manuel Amoros amepewa mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Benin. Rais wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo Moucharafou Anjorin amesema kuwa Amoros ndiye mgombea na baada ya kusafiri kuelekea jijini Cotonou alikubali kusaini mkataba huo utakaomuwezesha kumuweka nchini humo mpaka 2014. Amoros ambaye ana miaka 50 aliwahi pia kwa kipindi kifupi kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Comoros mwaka 2010 na wakati akiwa mchezaji aliwahi kushiriki mara mbili michuano ya Kombe la Dunia na pia alikuwemo katika kikosi cha Ufaransa kilichonyakuwa Kombe la Ulaya mwaka 1984. Mchezo wa kwanza akiwa kocha wa Benin uwakuwa ni dhidi ya Ethiopia Februari 29 mwaka mchezo ambao utakuwa ni wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.
No comments:
Post a Comment