Sunday, February 12, 2012

HENRY KUREJEA NY RED BULL BAADA MKOPO KUISHA.

MSHAMBULIAJI wa New York Red Bulls Thierry Henry aliyekuwa kwa mkopo katika klabu ya Arsenal anatarajiwa kurejea katika klabu yake hiyo ya Marekani mara muda wa mkopo wake wa miezi miwili na klabu hiyo ya Uingereza utakapomalizika. Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alikuwa akifikiria kuongeza muda wa wiki mbili baada ya mkopo wa miezi miwili kumalizika kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa lakini amesema kuwa hilo haliwezekani. Mchezaji amebakisha mchezo mmoja kuichezea klabu yake hiyo ya zamani dhidi ya AC Milan katika mchezo wa Klabu Bingwa ya Ulaya Februari 15 kabla hajarejea katika klabu yake ya NY Red Bulls Februari 16. Henry amefunga mabao matatu katika michezo sita ambayo ameingia akitokea benchi la wachezaji wa akiba ambapo ameongoza idadi ya mabao aliyofunga akiwa Arsenal na kufikia 229 kutoka 226.

No comments:

Post a Comment