Sunday, February 12, 2012

FERGUSON AMBWATUKIA SUAREZ.

MENEJA wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson amembwatukia mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez kwa kukataa kushikana mikono na Patrice Evra akisisitiza kuwa mshambuliaji huyo hafai kuichezea Liverpool tena. Mabao mawili yaliyofungwa na mshambuliaji wa United Wayne Rooney kabla ya bao moja la kufutia machozi lililofungwa katika dakika za majeruhi na Suarez yaliipa United ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool katika mchezo uliojawa na kila aina ya upinzani kutoka kwa wachezaji wawili Evra na Suarez. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Ferguson amesema kuwa hakuamini kitendo kilichotokea kwakuwa alikuwa tayari ameshaongea na Evra katika vyumba vya kubadilishia nguo kuhusiana na suala hilo na alikubali kumshika mkono mchezaji huyo. Ferguson aliendelea kusema kuwa kitendo kilichofanywa na Suarez cha kukataa kumshika mkono Evra ni cha aibu kubwa kwa klabu kama Liverpool na kwa maono yake hadhani kama mchezaji huyo anastahili kuichezea klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment