Sunday, February 12, 2012

ROMARIO AIKOSOA NCHINI KUTOKANA NA MAANDALIZI MABOVU YA KOMBE LA DUNIA.

NYOTA wa zamani wa Brazil Romario kwa mara nyingine ameikosoa nchi yake katika maandalizi ya Kombe la Dunia mwaka 2014 kwa kusema kuwa anahofia aibu kufuatia ujenzi wa kusuasua katika viwanja vya ndege. Romario ambaye kwasasa ni mbunge amesema kuwa kutakuwa na matumizi yaliyozidi katika viwanja 12 vitavyotumika kwa ajili ya Kombe la Dunia na itawabidi wachukue fedha za umma na kuitumia michuano hiyo kama sababu. Katika mahojiano yake na mtandao mmoja nchini humo Romario amesema kutakuwa na vurugu katika viwanja vya ndege nchini humo katika kipindi cha michuano hiyo kama ujenzi wa kuvikarabati viwanja hivyo hautaanza mapema. Nyota huyo amesema kuwa kama hatua za makusudi za ukarabati wa viwanja vya ndege hautafanyika haraka ni wazi kwamba nchi hiyo itatia aibu kutokana na ubovu wa viwanja hivyo akitolea mfano jinsi zinavyokuwepo vurugu katika kipindi cha mapumziko ambapo wageni wengi huingia nchini humo. Mbali na Romario nyota mwingine wa zamani wa nchi hiyo Pele naye alikuwa na mawazo kama hayo akidai kuwa viwanja vya ndege nchini humo vinahitaji ukarabati ili viweze kupokea wageni wengi katika kipindi cha michuano ya Kombe la Dunia.

No comments:

Post a Comment