Friday, February 3, 2012
JOHANSSON AMUOMBA BLATTER KUJIUZULU.
RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA Lennart Johansson ametuhumu rais wa Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA kuongoza kimabavu na kumuhitaji kujiuzulu wadhifa huo. Johansson mwenye miaka 82 ambaye aliwahi kuwa makamu wa rais wa FIFA alishindwa katika uchaguzi wa mwaka 1998 akigombea nafasi ya urais wa FIFA ambapo alikuwa akigombania na Blatter na toka kipindi hicho amekuwa madarakani mpaka leo. Akihojiwa Johansson ambaye ni raia wa Sweden amesema lazima kufanyike mabadiliko ndani ya Shrikisho hilo ambalo kwa siku za karibuni limekumbwa na changamoto kubwa za rushwa. Rais huyo wa zamani wa UEFA anaamini kuwa rais wa sasa wa UEFA Michel Platin ndiye anayefaa kukalia kiti cha Blatter akidai kuwa Platin amefanya mengi kwa Ulaya na ataweza kuibadilisha FIFA na kurudi katika hali yake ya kawaida.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment