Friday, February 10, 2012
MAREKANI KUCHEZA NA JAPAN NA BRAZIL.
TIMU ya taifa ya mpira ya wanawake ya Marekani inatarajia kucheza michezo miwili dhidi ya Japan na Brazil Aprili mwaka huu. Mchezo wa kwanza utachezwa Aprili moja dhidi ya mabingwa wa Kombe la Dunia Japan jijini Sendai nchini humo na wa pili utachezwa Aprili 3 dhidi ya Brazil jijini Chiba katika michuano mipya ya Kombe la Kirin. Akihojiwa kocha wa Marekani Pia Sundhage ambaye alikiwezesha kikosi hicho kushika nafasi ya pili katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana amesema kuwa kucheza na timu zenye viwango bora duniani ni changamoto kubwa lakini atajitahidi kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano hiyo. Kabla la kwenda nchini Japan kwenye michuano hiyo timu inatarajiwa kuelekea nchini Ureno kushiriki michuano ya Kombe la Algarve ambapo wameshanyakuwa taji hilo mara nane katika kipindi cha nyuma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment