Friday, February 10, 2012

PELE ASISITIZA HAKUNA MCHEZAJI ATAKAYEMFIKIA.

MCHEZAJI nguli wa zamani kutoka Brazil Pele amesisitiza kuwa hakutatokea mchezaji mwingine anayefanana nae duniani. Kauli ya nyota huyo imekuja wakati akizundua sanamu la sura yake katika uwanja wa L’Amitie jijini Libreville uwanja ambao ndio utachezwa mchezo wa fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili. Katika uzinduzi huo Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba alimtania Pele akiuliza nani ni bora kuliko mchezaji huyo akijibu swali hilo kwa utani Pele amesema kuwa kuona Pele mwingine akizaliwa itakuwa ngumu labda kutakuwa na mchezaji mwingine bora zaidi ya Pele na anayefanana na Pele lakini Pele mwingine haitawezekana kwakuwa wazazi wake walishafunga kizazi zamani sana. Katika uzinduzi huo Pele pia alikumbuka wakati alipokuja nchini humo kwa ziara na timu ya Santos mwaka 1967 wakati kukiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo ambapo kiongozi wa wakati huo alikuwa baba wa rais wa sasa Ali Bongo ambaye alikuwa akiitwa Omar Bongo. Pele amesema kuwa rais wa kipindi hicho Bongo alisimamisha vita kwakuwa walikuwa wakitaka kumuona Pele akicheza na walifanya hivyo wakacheza halafu wakaondoka ilikuwa ni kumbukumbu nzuri sana.

No comments:

Post a Comment