Wednesday, February 1, 2012
MENSAH FITI KUIVAA GUINEA.
NAHODHA wa Ghana John Mensah anaamini kuwa atakuwa amepona ndani ya muda na kuwemo katika kikosi cha Ghana kitakachocheza mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Guinea. Katika mchezo huo Ghana itahitajika ishinde na kuongoza kundi lao ili ibakie jijini Franceville na nahodha huyo anadai sasa anajisiki vyema baada kuumia na kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Botswana. Mensah hakushiriki mazoezi na wenzake Jumapili asubuhi lakini anaweza kucheza baada ya kumaliza adhabu ya kufungiwa mchezo mmoja kutokana na kadi nyekundu aliyopewa ambapo kocha wa timu hiyo itabidi aumize kichwa baada ya kuwa na mabeki wa kati wanne. Nahodha huyo alitazama kikosi chake kilipoifunga Mali akiwa benchi na kusema kuwa amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu hiyo wakati yeye akiwa hayupo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment