Monday, February 13, 2012

RENARD AJIFANANISHA NA MOURINHO.

KOCHA wa timu ya taifa ya Zambia Herve Renard amejifananisha mwenyewe na kocha wa Real Madrid Jose Mourinho akijiita mteule. Kocha huyo raia wa Ufaransa ana kila sababu ya kuwa na furaha baada ya kuiongoza kikosi Zambia wanaojulikana zaidi kama Chipolopolo kunyakuwa taji lao la kwanza la michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2012. Timu hiyo ambayo inatoka katika ukanda wa Kusini mwa Afrika walifanikiwa kuifunga timu ambayo ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kunyakuwa taji hilo kutokana na nyota iliyosheheni ya Ivory Coast kwa changamoto ya mikwaju ya penati 8-7 jijini Libreville. Renard alichukua mikoba ya kuinoa Chipolopolo mwaka 2010 baada ya aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Dario Bennetti kubwaga manyaga ikiwa ni siku kabla ya michuano ya 28 ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huo.

No comments:

Post a Comment