Monday, February 13, 2012

ROONEY AMPIGIA DEBE GERRARD KUWA NAHODHA UINGEREZA.

MSHAMBULIAJI wa Manchester United Wayne Rooney amesema nyota wa Liverpool Steven Gerrard ndiye anafaa kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza. Kwasasa Uingereza hawana nahodha wala kocha baada ya aliyekuwa kocha wa nchi hiyo Fabio Capello kujiuzulu Jumatano iliyopita kufuatia John Terry kuvuliwa unahodha na Chama cha Soka cha nchi hiyo-FA. Hatua hiyo ya FA ilifikiwa kutokana na mchezaji huyo kusubiri kusikilizwa kwa kesi yake iliyotokana na kutoa kauli ya kibaguzi lakini mchezaji huyo ataweza kuitumikia nchi yake katika michuano ya Kombe la Ulaya itakayochezwa baadae mwaka huu. Rooney aliandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa kama akiteuliwa kuwa nahodha wa Uingereza atafurahia lakini akasema suala hilo ni juu ya kocha mpya atayeteuliwa ingawa kwa muono wake yeye anaona Gerrard anafaa zaidi kwa nafsi hiyo.

No comments:

Post a Comment