BLATTER NAE AOMBA RADHI SERIKALI YA BRAZIL.
|
Makao Makuu, FIFA |
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter ameomba radhi kufuatia kauli ya Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Jerome Valcke kuhusu maandalizi ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Kauli hiyo ya Blatter imekuja kwa barua kwenda serikali ya Brazil ikiwa ni siku moja baada ya Valcke nae kuomba msamaha kwa kauli yake aliyoitoa. Serikali ya nchi hiyo iliwafahamisha FIFA kuwa hatafanya kazi na Valcke baada ya kauli yake ambayo ilileta hisia tofauti, ambapo bado haijafahamika kama serikali hiyo itakubali msamaha huo na kuamua kuendelea kufanya kazi na Valcke. Serikali imesema kuwa Waziri wa Michezo Aldo Rebelo atajibu barua hiyo kutoka FIFA kwanza kabla ya kutangaza uwamuzi wake hapo baadae.
No comments:
Post a Comment