Tuesday, March 6, 2012
GAMBIA YAONYWA NA FIFA.
SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limeionya nchi ya Gambia baada ya serikali ya nchi hiyo kutengua uongozi wa soka kufuatia timu hiyo kufungwa katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Katika taarifa yake FIFA imesema kuwa haitafanya kazi na uongozi mpya ambao umewekwa na Wizara ya Vijana na Michezo ya nchi hiyo. FIFA imewataka viongozi walioenguliwa na wizara hiyo kuwasilisha maelezo yao ifikapo Alhamisi kabla ya kuamua kupeleka suala hilo katika Kamati ya Dharura ya FIFA ambayo inasimamiwa na rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter. Jopo linaloongozwa na Blatter lina uwezo wa kuifungia nchi kushiriki katika mashindano yoyote duniani kama serikali husika itaonekana kuingilia masuala ya uongozi wa michezo. Wizara ya Vijana na Michezo ya nchi hiyo iliwatimua viongozi wa Shirikisho la Soka la nchi hiyo-GFA Ijumaa iliyopita baada ya timu ya taifa kufungwa na Algeria kwa mabao 2-1 katika mchezo ambao timu hiyo ilikuwa nyumbani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment