Tuesday, March 6, 2012
ARSENAL YAFA KIUME.
TIMU ya AC Milan imefanikiwa kutinga hatua robo fainali ya michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya pamoja na kufungwa na Arsenal katika mchezo wa pili wa michuano hiyo kwa mabao 3-0. Katika mchezo wa kwanza AC Milan wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa San Siro walifanikiwa kuwafunga Arsenal mabao 4-0 hivyo kufanikiwa kuingia katika hatua hiyo kwa idadi ya mabao 4-3. Mabao ya Arsenal katika mchezo huo yalifungwa katika kipindi cha kwanza na Laurent Koscielny kwa kichwa, Tomas Rosicky akitumia vyema makosa ya mabeki wa Milan na Robin van Persie aliyefunga bao la tatu kwa nia ya penati baada ya mshambuliaji Alex Oxlade-Chamberlain kuangushwa katika eneo la hatari. Mchezo mwingine uliochezwa jana ulishuhudia Benfica wakisonga mbele baada ya kufanikiwa kuwafunga Zenit St Petersburg kwa mabao 2-0 na kuifanya timu hiyo kuingia robo fainali kwa idadi ya mabao 4-3. Michuano hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo ambapo mabingwa watetezi wa michuano hiyo Barcelona watajitupa uwanjani kupambana na Bayer Leverkusen katika Uwanja Camp Nou ambapo katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Ujerumani Barcelona walishinda mabao 3-1. Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Apoel Nicosla ambao wataikaribisha Lyon ambao katika mchezo wa kwanza walifanikiwa kushinda bao 1-0.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment