Tuesday, March 6, 2012
VALCKE AOMBA RADHI SERIKALI YA BRAZIL KWA KAULI YAKE.
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Jerome Valcke ameiomba msamaha Brazil Jumatatu baada ya serikali ya nchi hiyo kulifahamisha shirikisho hilo kuwa ahwahitaji kufanya kazi na katibu huyo kufuatia kauli yake kuhusu maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2014. Katika taarifa yake aliyoituma kwa Waziri wa Michezo wa Brazil Aldo Rebelo, Valcke amesema kauli yake ambayo ilitafsiriwa kutoka lugha ya kifaransa kwenda kireno imekuwa na maneno makali zaidi ya alivyosema. Msamaha huo umekuja baada ya Brazil kuandika barua iliyosainiwa na Rebelo kwenda kwa rais wa FIFA Sepp Blatter kuwa nchi hiyo haihitaji kufanya kazi na Valcke. Valcke aliomba msamaha kwa Rebelo na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine walichukizwa na kauli yake lakini alijitetea kuwa maneno hayo yamekuwa makali zaidi yalipotafsiriwa kwa kireno kuliko yale halisi aliyozungumza kwa kifaransa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment