Thursday, March 15, 2012

CASILLAS KUFUNGA NDOA NA CARBONERO.

GOLIKIPA wa klabu ya Real Madrid Iker Casillas anatarajiwa kufunga ndoa na rafiki yake wa kike wa muda mrefu Sara Carbonero Julai mwaka huu baada ya michuano ya Kombe la Ulaya. Casillas mwenye umri wa miaka 30 na Carbonero ambaye ana miaka 28 wamekuwa pamoja katika kipindi ccha miaka mitatu sasa ambapo nahodha huyo wa klabu ya Madrid ameshamchumbia rafiki yake huyo zaidi ya mara moja. Gazeti moja la habari za udaku nchini humo lilidai katika kipindi chote ambacho Casillas amekuwa akimchumbia binti huyo amekuwa akikataa lakini mwishoni sasa amekubali ingawa hakuna taarifa zaidi kuhusiana na suala hilo. Wawili hao wote wanatarajiwa kuwepo nchini Poland na Ukraine kuanzia June 8 mpaka Julai 1 ambapo kutafanyika michuano hiyo ambayo Casillas anatarajiwa kuwepo langoni ili kukiongoza kikosi chake kutetea ubingwa huo ambao waliutwaa mwaka 2008, huku Carbonero yeye atakuwa akitangaza michuano hiyo katika moja ya televisheni za binafsi nchini Hispania.

No comments:

Post a Comment